Picha zaonesha 'wizi' wa kura Sudan ![]() | ||||
Wanaharakati wa upinzani nchini Sudan wamesema, picha ya video iliyosambazwa kwenye tovuti inathibitisha madai yao ya udanganyifu katika uchaguzi. Wanaharakati hao wanasema video hiyo inaonesha maafisa wa uchaguzi wakitumbukiza karatasi ndani ya maboksi ya kupigia kura. Picha hiyo, ambayo hata hivyo haijathibitishwa rasmi, imewekwa kwenye tovuti na inasambazwa na kundi mpja la wanaharakati. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema picha hiyo si ya kweli na haitafanya uchunguzi wowote juu yake. Uchaguzi huo ulifanywa kufuatia makubaliano ya amani ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 20. Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutolewa wiki hii. |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa