Translate in your language

Tuesday, April 13, 2010

 

VIFO VYA AKIMAMA VYAPUNGUA KWA THELUTH MOJA DUNIANI

 
Utafiti mpya umeonyesha maendeleo ya kuridhisha katika kupunguza idadi ya vifo vya wanawake duniani, wakati wa ujauzito au kujifungua.
 

Utafiti huo ambao umechapishwa hivi karibuni umesema vifo hivyo vimepungua kwa karibu theluthi moja ikilinganishwa na idadi ya mwaka 1980, ikiwa ni mafanikio zaidi ya ilivyotarajiwa.

 

Na inaaminiwa kuwa matokeo hayo yanaonyesha mafaniko katika kuafikia malengo ya milenia mwaka 2015.

Miongoni mwa nchi ambazo zilipiga hatua kubwa ni China, Misri, Ecuador na Bolivia.

 

Lakini vifo vya akina mama wajawazito au wanaojifungua vilipanda katika baadhi ya nchi ikiwemo Marekani


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)