| UCHAGUZI SUDAN WAINGIA ZENGWE WASOGEZWA MBELE ![]() Mariam Almahdi | ||||
| Shughuli ya upigaji kura inaendelea leo nchini Sudan kwa siku ya tatu ingawa tume ya uchaguzi imeongeza muda wa shughuli hiyo, kwa siku zingine mbili na kufikisha tano siku kamili za upigaji kura. Uamuzi huo uliafikiwa baada ya kuripotiwa matatizo kadhaa kwenye shughuli hiyo. Vituo kadhaa vya kupigia kura vilifinguliwa kuchelewa, baadhi vikiripotiwa kutokuwa na karatasi za kutosha za kupigia kura na vingine vikiwa na makaratasi yasiyokubalika. Hata hivyo vyama kadhaa vya upinzani, vikiwemo vile vilivyoususia uchaguzi, tayari vimedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya udanganyifu. Hususan vimeshtumu Marekani kwa kuonekana kukubali kuwa uchaguzi ulikuwa shwari licha ya kuripotiwa dosari. Msemaji wa chama cha Umma, Mariam al-Mahdi, alimshutumu mjumbe maalum wa Marekani nchini humo Scott Gration, kwa kuwapuuza raia wa Sudan | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa