Uwanja wa Heathrow wafunguliwa ![]() | ||||
Ndege hatimaye zimeanza kutua na kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London, ambao ndio uwanja wenye shughuli nyingi zaidi barani ulaya, baada ya uingereza kuondoa vikwazo dhidi ya usafiri wa ndege. Marufuku hiyo imekuwepo tangu mlipuko wa volcano nchini Iceland wiki moja iliopita. Nchi kadhaa pia zimelegeza vikwazo vya usafiri wa ndege lakini katika mataifa mengine marufuku hiyo bado inaendelea kudumishwa. Nusu ya idadi ya safari za ndege zilirejelewa jana na maelfu ya abiria bado wamekwama katika viwanja kadhaa vya ndege duniani. Mlipuko huo wa Volcano nchini Iceland unaendelea lakini viwango vya mawingu ya majivu vimepungua. |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa