Translate in your language

Wednesday, April 7, 2010



Nigeria yawaapisha mawaziri wapya
 

Goodluck Jonathan amewatimua takriban wote ambao Wanigeria wanawaita, wanachama wa genge.


Watu hao walikuwa ni marafiki wakubwa wa Rais Yar'Adua ambao walifanya juu chini kuhakikisha anasalia madarakani hata alipoonekana taabani na kushindwa kutia saini nyaraka za serikali.


Kaimu rais amewateua watu wapya kabisa wenye utiifu kwake, mmoja akiwa ni Olusegun Aganga, afisa mwandamizi wa benki ya uwekezaji ya Goldman Sachs kuwa waziri wa fedha.


Yeye anaonekana kama mwanamageuzi anayetazamiwa kuunga mkono sera za uwazi na vita dhidi ya ufisadi.

Lakini pia ameweka mizani ambapo mawaziri wachache wa serikali ya Yar 'Adua wamesalia na hata amemteua mpwa wa Yaradua katika uwaziri.


Hatua hiyo imeigawanya familia ya Yaradua na kuwavutia baadhi ya jamaa zake kuwa upande wa Jonathan.

 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)