Uchaguzi Uingereza kufanyika Mei | ||||
Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown,ametangaza kuwa uchaguzi mkuu utafanyika tarehe sita Mei.
Gordon Brown Aliyatangaza hayo baada ya kwenda katika kasri ya malkia wa Uingereza kuomba kibali cha kulivunja bunge. Chama chake cha Labour kinajaribu kutafuta ushindi wa muhula wa nne mfululizo. Bw Brown amesema anaomba ridhaa kutoka kwa wananchi wa Uingereza aendelee na kazi ya kufufua uchumi. Viongozi wa upinzani, David Cameron wa chama cha Conservative na Nick Clegg wa chama cha Liberal Democrat wamehimiza kufanyike mageuzi. Hii itakuwa ni kampeni ya kwanza ya Bwana Brown tangu ashike wadhifa wa waziri mkuu baada ya kuchukua uongozi wa chama cha Labour kutoka kwa Tony Blair miaka miwili iliyopita na utakuwa wa kwanza kushuhudia mdahalo kati ya viongozi wa vyama vikuu. Maswala ya kodi na matumizi yanatazamiwa kutawala kampeni hizi wakati Uingereza inajaribu kupunguza nakisi yake kubwa ya bajeti. | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa