Julius Malema aonywa na ANC ![]() | ||||
Chama tawala nchini Afrika kusini ANC, kimemuonya kiongozi wa vijana wa chama hicho Julius Malema, dhidi ya kutoa matamshi yenye kuzua hisia kali. Onyo hili linafuatia kauli ya Malema kuwa 'Wazungu wauawe', ambayo wengi wanasema ulisababisha kuuawa kwa mwanasiasa mzungu Eugene Terre'blanche aliyeunga mkono siasa za ubaguzi wa rangi. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa chama Gwede Mantashe, walikutana na Malema pamoja na rais Jacob Zuma na kumuonya kukoma kuimba nyimbo za enzi ya ubaguzi wa rangi. Malema aliwahi kuonywa na mahakama kutoimba wimbo huo ambao wafuasi wa marehemu Terre'blanche wanasema ulichochea mauaji yake. | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa