| Muungano wa Ulaya wakosoa uchaguzi wa Sudan | ||||
| Muungano wa Ulaya, ambao umekuwa ukifuatilia uchaguzi nchini Sudan, umesema kuwa uchaguzi ulishindwa kufikisha viwango vya kimataifa. Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa EU, Veronique de Keyser, aliviambia vyombo vya habari kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Khartoum, kuwa uchaguzi uliweza kutimiza vigezo vichache muhimu. Shughuli ya kuhesabu kura nchini Sudan inaendelea, ukiwa ni uchaguzi wa kwanza wenye kushirikisha vyama vingi kuwahi kufanyika katika kipindi cha takriban robo karne. Vyama kadhaa vya upinzani vilisusia uchaguzi kwa madai ya wizi kura. Malalamiko ya hivi karibuni yametolewa na mgombea wa kiti cha urais kutoka kambi ya upinzani, Abdelaziz Khaled, ambaye aliwashtumu maafisa wa uchaguzi kwa kusimamia shughuli ya upigaji kura katika hali ya kuwepo kwa machafuko. Wakaguzi kutoka Kituo cha Carter, kikundi kinacho-ongozwa na rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, pia wanatarajiwa kutoa repoti yao juu ya uchaguzi huo. | ||||
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa