Translate in your language

Saturday, April 17, 2010

 

MBUNGE SINGIDA MJINI AMSAIDIA MWANANCHI WAKE GHALAMA ZA MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO INDIA

 Flora Francis(21) akiwa makao makuu ya ofisi za METL, muda mfupi kabla ya safari ya kwenda India

 

MBUNGE wa jimbo la Singida Mjini Mohammed Gulamu Dewji  juzi aliweza kufanikisha safari kwa mwancdhi wa jimbo lake kupatiwa matibabu ya upasuaji wa ugonjwa wa noyo nchini India.

 

Dewji alitimiza adhima ya safari hiyo kwa kazi huyo mkazi wa Singida mjini, Flora Francis (21) ambaye aliweza kumsaidia matibabu kwa kipindi cha miezi kadhaa mpaka kufanikishiwa safari ya matibabu.

 

"Nashukuru ofisi ya Mbunge wa jimbo la Singida mjini  kwa msaada niliyopatiwa kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa moyo, nimeteseka kwa muda mrefu hali na familia yetu haikuwa na uwezo' alisema Frola.

 

Kwa upande wa mama mzazi wa Frola, Magdalena Francis alishukuru kwa msaada huo huku akitanguliza shukrani zake kwa Dewji kwa msaada huo. "Tunahamini kwa safari ya kwenda India itaweza kusaidia na kumpunguzia tatizo lake hilo" alisema mama mzazi.

 

Mgonjwa huyo Flora Francis alipatwa na tatizo hilo  mwaka mmoja nyuma baada ya kugundulika alipokuwa mjamzito, hali ambayo alipopimwa Muhimbili aligundulika kuwa na matatizo ya Moyo katika mfumo wa upumuaji.

 

Safari hiyo ya kwenda India kwa matibabu, mgonjwa huyo aliongozana na wagonjwa wengine 24 chini ya uratibu wa  Hospitali ya Regency na  (Heart Surgery Project Lion) Lions Club,inayoongozwa na  Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency, Dr Rajni Kanabar.

 

Kwa upande wake Dr Rajni Kanabar alisema kuwa, baada ya kupatiwa matibabu wagonjwa hao wanatalajia kurudi Tanzania baada ya wiki nne hadi tano.

 

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)