| Volkano yaendelea kukwamisha usafiri wa anga ![]() | ||||
| Sehemu nyingi za bara Ulaya zitaendelea kukosa usafiri wa ndege mpaka alfajiri ya Jumamosi kutokana na anga kujaa majivu ya volkano yanayotimka kutoka Iceland, maafisa wameeleza. Sehemu kubwa ya anga la safari za ndege maeneo mengi ya Ulaya kaskazini na magharibi limefungwa, huku pungufu ya nusu ya idadi za safari za ndege zikifanyika Ijumaa. Maelfu ya abiria barani Ulaya na kote duniani wameathirika kutokana na athari za majivu hayo ambayo yanadaiwa yanaweza kuharibu injini za ndege zinapokuwa angani. Wanasayansi wanasema volkano bado inatimka ingawa inatoa majivu kidogo ikilinganishwa na mwanzo. Volkano ya Eyjafjallajokull ilianza kulipuka siku ya Jumatano kwa mara ya pili mwezi huu na kurusha majivu umbali wa kilometa 11 kwenda angani. | ||||

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa