Translate in your language

Thursday, April 1, 2010

KOMBE LA NYALANDU



MTIKO STARS YANYAKUWA KOMBE LA MBUNGE NYAULANDA

mbunge- Nyaulanda

Timu ya soka ya Mtinko Stars imekabidhiwa shilingi laki tano baada ya kutawazwa kuwa mabingwa wa kombe la Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu kwa kuwafunga majirani zao,timu ya Ilongero Star kwa jumla ya mabao 4 bila majibu.

 

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye viwanja vya michezo vya shule ya msingi ya Malolo,wenyeji wa mchezo huo Mtinko walianza kuzichana nyavu za Ilongero katika dakika ya 33 bao lililofungwa na John Andrea.

 

Ilikuwa ni katika dakika ya  39 baada ya kupokea krosi murua kutoka kwa Saidi Abrahamani na kumkuta Ramadhani Omari ambaye bila ajizi aliachia shuti kali lililoenda moja kwa moja kwenye lango la wapinzani wao na kuandika bao la pili.

 

John Andrea aliipatia timu yake bao la tatu lililopatikana katika dakika ya 44 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Ilongero, mabao ambayo hata hivyo yaliyodumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.

 

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji,mabadiliko ambayo hayakuweza kubadili sura ya mchezo huo uliohudhuriwa na idadi kubwa ya wapenzi na washabiki wa mchezo huo wa soka.

 

Mchezaji  Mussa Omari alipigilia msumari wa moto na kuandika bao la nne katika dakika ya 65 kipindi cha pili.

 

Hata hivyo Ilongero Star watalazimika kujilaumu wenyewe kwani licha ya kupata penelti lakini hawakuweza kuitumia vyema.

 

Kutokana na matokeo hayo Mtinko Star wameshika nafasi ya kwanza na Ilongero kuwa washindi wa pili katika ligi hiyo na hivyo kukabidhiwa zawadi ya shilingi laki tatu.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu alifafanua kuwa baada ya kudhamini ligi hiyo anatarajia pia kudhamini michezo mingine kama vile riadha na mpira wa miguu.

 

Wakizungumzia machezo huo kocha wa timu ya Mtinko star,Abdala Goda alisema siri ya ushindi huo inatokana na mazoezi ya nguvu waliyokuwa wakifanya wakati kocha wa Ilongero star Issa Juma Muro licha ya kukubali matokeo lakini alisema vijana wake walizidiwa na ugeni wa uwanja

 


 

 

 




No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)