Translate in your language

Thursday, April 1, 2010

Fw: NYALANDU AWAPONGEZA UVCCM


NYAULANDA AWATAKA VIJANA KUWA NA MOYO WA UJASILIAMALI
Mbunge wa Singida Kaskazini-Lazaro Nyaulanda


Vijana nchini wamekumbushwa wajibu wao wa kufanyakazi kwa bidii,kwa kujituma na kwa maarifa ili waweze kujiongezea kipato,badala ya kuendelea kulalamikia hali ngumu ya uchumi.

 

Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Bwana Lazaro Nyalandu aliyasema hayo alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Hosteli ya jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Singida.

 

Aidha Nyalandu alibainisha kuwa vijana wa mkoa huo bila kujali itikadi za vyama vyao wajifunze kufanyakazi kwa bidii,ubunifu na kwa ushindani.

 

Kwa mujibu wa Nyalandu anachoamini kwa vijana hao ni moyo wa ujasiriamali kwa hali hiyo vijana hao hawana budi kutambua kuwa taifa la Tanzania lipo kwenye ushindani na vijana singida watapiga hatua mbele tu iwapo wakijua ushindani ndiyo unalolifanya taifa lisonge mbele.

 

Hata hivyo Nyalandu ambaye pia ni naibu kamanda wa UVCCM Mkoa alisema jengo hilo lenye jumla ya zaidi ya vyumba 23 litakuwa kwa ajili ya kituo cha mafunzo ya kompyuta,internet yatakayowasaidia vijana hao kusonga mbele.

 

Naye Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Paschal Kurwa Mabiti alisema serikali mkoani hapa ipo katika hatua za mwisho mwisho za kukamilisha utaratibu wa kuanzisha mfumo wa masomo kwa kutumia mtandao wa internet.

 

Akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo mkandarasi wa jengo hilo ,Bwana Emmanueli Wami alisema mpaka sasa wamekwishatumia shilingi milioni sitini na kwamba hadi litakapokamilika linatarajia kugharimu shilingi milioni 75.

 


 







No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)