Translate in your language

Saturday, March 20, 2010

ZIARA YA USIMAMIZI ZOEZI LA UGAWAJI WA VYANDARUA VISIWANI MAFIA

Ziara yetu ilikuwa ni usimamizi kuhakikisha kuwa zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa watoto chini ya miaka mitano linafanikiwa kwa utaratibu mzuri uliopangwa na Serikali, ziara yetu ilikuwa kutembelea visiwa vilivyo ndani ya kisiwa cha MAFIA navyo ni:- JIBONDO, JUANI na CHOLE
safari ilikuwa kama ifuatavyo:- safari yetu ilianza mnamo saa 3:47 asubuhi kwa kupanda boti
 eneo la UTENDE

na huyu jamaa ndie alikuwa pilot wetu
tulianza  juani kisha chole na kumalizia jibondo

zoezi likiwa linaendelea la ugawaji wa vyandarui ivyo na mama akionekana akiweka sahihi baada ya kuchukua chandarua
watoto Mariam na Abdul wakiwa tayari wamepewa vyandaruavyao tayari kwa kujilinda na Malaria

Baada ya kutoka juani tulielekea kisiwa cha Chole 
maji yalikuwa yametoka ivyo ikatulazimu tushuke mbali kidogo, kama ukiangalia vizuri kwa nyuma yangu utaona mwenzangu anakuja na pia boti tuliokuwa tunaitumia kusafiria

na hawa nao walikuwa wenzangu katika safari hii


haya ni baadhi tu ya MANDHARI MAZURI ya kisiwa cha CHOLE 


watoto Mussa Ahmadi na huyu mrembo ambaye sikuwai kupata jina lake wakiwa wameshikilia vyandarua vyao katika kisiwa cha Chole 



snapz za kisiwa cha Jibondo 
tambarare nzuri na hali ya utulivu wa kisiwa cha Jibondo
 
aisee bahari noma hapa ni baadhi ya maeneo yakiwa yameliwa na bahari, na mwenyeji wetu ametuleza kuwa kuna makaburi ya zamani yamechukuliwa na bahari na picha ya mwiso ni msikiti wa zamani ukiwa unachukuliwa na bahari baadhi ya upande wake 

NA HII ilikuwa safari ya kurudi baada ya kufanikisha ziara yetu hii katika usimamizi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa watoto walio chini ya miaka mitano katika visiwa vya chole, juani na jibondo wilayani MAFIA




KARAIBUNI SANA MAFIA KUENJOY MANDHARI NZURI YA VISIWA NDANI YA VISIWA KWANI KUNA HALI NZURI YA HEWA PAMOJA NA HISTORY NZURI ZA KUFURAHISHA NA AKUFUNDISHA 

na hiyo ndiyo safari yetu kwa ufupi


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)