Breakin News!!
TRAWU,NAO WATANGAZA MGOMO KUUNGANA NA TUCTA Na Mwanablog wetu Dar CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu) imetoa tamko rasmi ya kuunga mkono mgomo uliotangazwa na Chama cha Wafanyakaazi Nchini (TUCTA) wa kugoma nchi nzima. Akizungumza na waandishi wa Habari jana, jijini Rwegasira alisema kuwa, wao "Sisi hatujashinikizwa na mtu, bali kwa kuzingatia misingi ya katiba na tukiwa wanachama halali wa TUCTA, tumetangaza rasmi kuwaunga mkono, kwa kuchoshwa na mifuko ya hifadhi ya jamii, yakiwemo NSSF na PPF." Alisema Rwegasira. Kwa kile alichodai kuwa, mashirika hayo ndiyo chanzo kikuu cha kurudisha nyuma maswala yote ya wafanyakazi nchini, ikiwemo kufanya ufisadi mkubwa wa kuwakata makato makubwa pamoja na unmyonyaji mkubwa katika mishahara "Mashirika ya PPF na NSSF, yanaongoza kwa kukata makato makubwa ya wafanyakazi huku, lakini mfanyakazi anapokuja kustaafu, mafao yake anayolipwa hayaendani na hali halisi ya kutumikia kwake kufuatia mashirika hayo kukata makatio makubwa" alisema. Aliendelea kusema kuwa, mashirika hayo yamekuwa yakikata makato mengi na makubwa wafanyakazi ambao mishahara ambayo ni midogo, huku wakijinufaisha katika kujenga majengo makubwa yakiwemo vyuo na pamoja na miradi ya majengo, pamoja na kukopesha wabunge fedha za wavuja jasho ambazio wao wanazifanyia kazi za kifisadi" alisema Rwegasira. |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa