Translate in your language

Friday, March 19, 2010

MUME AUA MKEWE.KISA KWA KUPIKA UGALI MWINGI


Na timu ya Blog Kagera




MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Reticia Protus (22) mkazi wa kitongoji cha Omurungu, Kata ya Minziro, Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera, ameuawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na mumewe, kwa sababu ya kupika ugali mwingi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Salewi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mtuhumiwa kuwa ni Rutashobya Muyo, mkazi wa Minziro, wilayani humo.

Alisema Muyo alitenda kosa hilo Machi 12, mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika eneo la kitongoji cha Omurungu.

Kamanda Salewi alidai mtuhumiwa alichukizwa na tabia ya mke wake kupika chakula kingi ndipo alipochukua panga na kuanza kumkata sehemu mbalimbali za mwili.

Hata hivyo, Kamanda Salewi alisema baada ya mtuhumiwa kutenda kosa hilo alitoweka na kwenda kusikojulikana, hali iliyosaidia marehemu kupata mwanya wa kukimbilia kwa kaka yake, John Protus, huku akilia na kusema mumewe anamuua.

Aidha, Salewi alisema kuwa kaka wa marehemu kwa kushirikiana na majirani waliamua kumkimbza hospitali kwa matibabu lakini kabla hawajafika alifariki dunia.



1 comment :

Anonymous said...

Great post. I used to be checking constantly this weblog and I'm inspired!
Very helpful info particularly the final section :) I deal with such information much.
I used to be seeking this certain information for a very long time.
Thank you and best of luck.

Feel free to surf to my blog hack game of war with jailbreak

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)