MFUKO WA UCHUMI SINGIDA YAKOPESHA MILIONI 283 Na Mwanablog wetu Singida Mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia taasisi mbali mbali za kifedha umetumia shilingi milioni 283 kutoa mikopo kwa wananchi katika kipindi cha kuanzia januari hadi disemba,mwaka jana.
Hayo yamebainishwa na afisa wa serikali za mitaa wa Mkoa wa Singida,Bwana Wilbardi Marandu alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya mkoa huo kilichofaanyika mjini hapa.
Kwa mujibu wa Marandu taasisi zilizochangia kiasi hicho cha fedha ni pamoja na Pride (T) iliyotoa 100,000,000,Benki ya CRDB Ltd 143,000,000 na Mfuko wa vijana 40,000,000.
Aidha afisa huyo wa serikali za mitaa alitanabaisha kwamba mikopo hiyo ilitolewa kupitia vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ambapo wanachama 3,850 walinufaika na mikopo hiyo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida.
Hata hivyo Marandu aliweka wazi pia kuwa katika jitihada za kuiongezea nguvu serikali,shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) na Pride (T) katika programu zao za kawaida waliweza kutoa mikopo.
Alibainisha msimamizi huyo wa serikali za mitaa mikopo iliyotolewa kupitia vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) vikundi vya kiuchumi pamoja na watu binafsi ni 875,900,000 zilizotolewa na SIDO kwa wananchi 1,331 na Pride (T) Ltd iliyotoa 1,720,900 kwa wanufaika 2,811 na hivyo kufanya jumla ya shilingi 2,596,800,000 kwa wanufaika 4,142.
Kwa mujibu wa Bwana Marandu jumla ya mikopo yote iliyotolewa ni 2,879,800,000 kwa wanufaika 7,992 kuweza wajasiriamali kujikomboa kiuchumi.
"Kuna mikopo kama ifuatavyo kupitia vyama vya akiba na mikopo (Saccos) vikundi vya kiuchumi na watu binafsi "Hivyo kwa ujumla mikopo iliyotolewa ni shilingi 2,879,800,000 kwa wanufaika 7,992 kuweza ili wajasiriamali waweze kujikomboa kiuchumi"alisisitiza Marandu |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa