WANAWAKE nchini wametakiwa kuacha tabia ya kubaguana na badala yake wajenge moyo wa mshikamano pamoja na kushirikiana katika shughuli za maendeleo ili wautokomeze umaskini katika jamii.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na mke wa rais, Salma Kikwete, alipokuwa akizungumza na vikundi vya wanawake wajasiriamali na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Arumeru wakati wa ziara yake ya kuangalia shughuli za maendeleo ya wanawake kupitia taasisi yake ya WAMA .
Alisema maendeleo ya mwanamke yataletwa na mwanamke mwenyewe na iwapo wanawake wakipendana na kushirikiana wana uwezo mkubwa wa kuleta mageuzi ya maendeleo ya kiuchumi ambayo pia yatawasaidia kushika nafasi za uongozi wa ngazi za juu sawa na wanaume.
Alibainisha kuwa wanawake na wanaume wako sawa na kuwa bila mwanamke hakuna mwanaume na bila mwanaume hakuna mwanamke, hivyo aliisisitizia jamii kutambua ukweli huo huku akiitaka iache tabia ya mfumo dume unaomkandamiza mwanamke.
"Wanaume acheni ubabe wa kuwaonea wanawake na kuwanyima sauti ya kufanya maamuzi," alisema Mama Salma.
Mama Salma Kikwete, alitoa hundi ya fedha yenye thamani milioni 2 kwa UWT wilaya huku akiwasihi waanzishe vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) kwa lengo la kujiendeleza katika sekta ya ujasiriamali.
Alibainisha kuwa taasisi yake ya WAMA ina vitengo vinne vinavyoshughulikia elimu kwa mwanamke ambavyo ni pamoja na afya ya mama na mtoto, watoto yatima na uwezeshaji kwa vikundi vya wanawake.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa