Translate in your language

Sunday, March 28, 2010

LUKUVI APATA MPINZANI JIMBO LA ISIMANI

 
WILIAM LUKUVI

 

MSOMI wa Shahada ya Sayansi Siasa, Jamii na Utawala ya Chuo Kikuu Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Felix Mdesa(33) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo la Isimani linaloshikiriwa na Wiliam Lukuvi.

 

Akitangaza nia yake  hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mdesa alisema kujitosa katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.

 

"Mbunge anayeshikiria jimbo hilo ameweza kufanya mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia na kuwa na Haki ya msingi kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi waliokosa fursa mbalimbali" alisema Mdesa.

 

Mdesa ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa Malawi Cargo Centre (MCC LTD)  na mzaliwa wa Kata ya Kihesa iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani, alisema kuwa, aamesukumwa na vitu vingi sana ambavyo  mpaka sasa bado havijatekelezwa likiwemo swala Ujenzi wa lami kwa zaidi ya miaka 30.

 

"Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, hikiwemo na wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza wajibu" alisema Mdesa.

 

Kwa kujitokeza huko kunafanya idadi ya wagombea kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo, Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza.

 

 

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)