Richard Kiyabo
CHAMA cha Jamii (CCJ), kimefanya uzinduzi wa huduma ya kujiunga kuwa wanachama kwa kutumia ya ujumbe mfupi wa simu (Teknolohama).
Mwenyekiti wa chama hicho Richard Kiyabo alisema chama kimeamua kuanza kutekeleza katiba yake kwa vitendo hususani suala la kuendeleza sayansi na teknolojia kwa ajili ya kuwafikia Watanzania wowote popote walipo.
Alisema utaratibu huo mpya unakuwa historia nchini na Afrika mashariki kwa ujumla kwa kupata wanachama wake kwa njia ya elektronia au kwa maneno mengine teknohama yani teknolojia ya habari na mawasiliano.
"Hatua hii imefanikiwa kutokana na uzoefu wa nchi zingine na mafanikio yanayopatikana kutokana na mfumo huo."alisema Mwenyekiti Kiyabo.
Kiyabo alisema anawaomba Watanzania wote wapenda maendeleo na ustawi wa nchi hii wajiunge na chama chao hicho kwa wingi kwa kutumia utaratibu huo usiohitaji muombaji wa uanachama kutokwa na jasho na kusumbuka.
Aidha alisema wanaahidi kuwa watatoa taari za mara kwa mara kuhusu mafanikio ya utaratibu huo unavyokwenda na mafanikio yake.
Kiyabo aliongeza kwa kusema chama chake hakina wivu wala hulka ya ushindani wa kitoto hivyo inavihimiza vyama vingine kujiunga na mpango huo wa teknolojia hiyo ya kisasa kwa faida ya taifa letu kwa kutoa msaada wa kitaalam kwa chama chochote kinachohitaji utaalamu huo.
Naye Katibu Mwenezi wa chama hicho, Dickson Ng'hily alisema utaratibu huo ni rahisi kwa kila mwanachama anayetaka kujiunga na CCJ, popote pale alipo ikiwa ni shamba, nyumbani, safarini au sokoni.
Alisema wanatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno CCJ kwenda namba 15337, kisha neno Sajili*Jina kamili* Tawi ulipo*Jimbo*Mkoa mara utakapokamilisha hatua hizo baada ya majuma matatu mwanachama atapokea kadi yake alipo.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa