Translate in your language

Thursday, March 11, 2010

HIVI HUU UTARATIBU WA KUMPATA KOCHA WA TAIFA STARS TUMEUPATA WAPI?

Nimekuwa nikijuuliza sanaa kuhusu huu utaratibu wetu tunaoufanya sasa wa jinsi ya kumtafuta kocha wa kuja kufundisha soka hapa nchini, TFF kupitia katibu wake mkuu imetangaza nafasi za kazi kwa ajili ya kocha wa Taifa Stars ambaye atairithi nafasi ya Mbrazil wetu Macio Maximo ambaye mkataba wake  unategemea kumalizika July mwaka huu.
 
          Kwa mila na desturi za kiafrika za leo sio rahisi Mwanaume kutangaza kwa uma kuwa anataka kuoa na wanaweke wanaotaka kuolewa naye wajitokeze ili achague miongoni mwa waliojitokeza ni yupi anayempenda!!! Nasema mwanamke nzuri na mwenye akili timamu walai hawezi kujitokeza.  Tunachotakiwa na wewe muoaji kufuatilia ni mwanamke gani unayeona atakufaa kiumbo, kitabia n.k na kwanza utaratibu wa maongezi kupitia kwa wazazi wake au mshenga na hatimaye yeye mwenyewe na mwishowe kuoana hapo ndipo ndoa hiyo itadumu.  Leo sijui TFF imepata wapi wazo hili na utaratibu huu ambao sijawahi kuona dunia kote zaidi ya Tanzania .  Wakati mheshimiwa Jekaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani alipita kila wirara na kutoa maelezo na dira yake.   Ndani ya wizara ya michezo na utamaduni aliiagiza          TFF ifanye kila mbinu imtafute kocha sehemu yeyote duniani na serikali itamlipia, sijui nini kilichowasibu walichukuwa muda mrefu wa kumtafuta kocha nadhani mawazo yao na mchakato wao wa kupata kocha mnzuri na  atakaye kidhi mahitaji yetu ndiyo yaliyoonekana kuchelewa kidogo, hadi Mheshimiwa Rais alipowajia juu bado walishindwa kutekeleza adhama hiyo, ndipo Rais katika ziara yake nchini Brazil akakamilisha mipango ya kumpata kocha ndani ya nchi ambayo ina vichea wa  soka dunia naye si mwingine ila ni Macio Maximo.  Sasa nashangaa TFF sula la maximo la kuisha kwa mkataba wake liko wazi  nilidhani ni wakati muafaka ndani ya zaidi ya miezi  saba kumtafuta kocha atakayerithi mikoba ya mbrazil huyo. Wangemtafuta kocha kulingana na mazingira ya nchi yetu na mahitaji yetu kwa sasa na wakakaa naye wakamuelewesha naye akawaelewesha, sasa ndio hapo ninaposhangaa nani aliyewapa wazo hii la upumbavu mno, ambaye kocha mwenye akili yake  si rahisi kutuma maombi,  katika moja ya vitabu vyangu vingi nilivyonavyo vya mwalimu Julius Kambarage Nyerenyere cha TUMETOKA WAPI, TUKO WAPI, TUNAKWENDA WAPI ukurasa wa ishirini na tatu (23) kwa maneno yake mwenyewe anasema “watu tunaafikiana na wazo lakini mawazo ambayo wazi wazi ni ya kijinga  lazima tuyakatae kwa sababu mtu yeyote mwenye akili akipata mawazo ya kipumbavu na wewe una akili na unajua ni ya kipumbavu na ukayakubali anakudharau”, sasa hayo maneno  ya baba wa Taifa yanatisha neno watu waliovua shauri TFF kama hii wanasiasa, au wanauchumi, au nje ya nchi kuwa sasa wako kimya nadhani wametudharau. Upo uwezekano hao hao ndio waliotushauri hata leo tuwe na ligi ya vodacom mbovu kuliko zote nilizopata kuziona, mchezaji wa Kitanzania kwa mwaka amecheza ligi miezi sita tu na sita mingine yote yuko likizo anaishia kucheza ndondo tu. FIFA wanataka mchezaji ili afikie kiwango kizuri cha kimataifa ni lazima acheze mechi zisizopungua 40 na si vinginevyo, leo TFF mchezaji wa ligi ya vodacom anayeweza kucheza mechi zote kwa muda wa miezi  yote sita anacheza mechi 22 tu ni ajabu na kichekesho kweli !!!!!.
          Watanzania leo wako kimya wanawashangaa TFF na utaratibu huo wa kumpata kocha lakini wengine wanadhani TFF inadanganya toto inaye iliemuandaa kocha wa timu ya Taifa si kocha wa TFF ni kocha wa wanchi na vyema wadau wa michezo wakawekwa wazi kuhusu ujio wake na wakamtambua mapema kabla ya kupewa kiti hicho cha stars.  Ni jukumu lenu TFF kutafuta kocha atakayelingana na matakwa ya nchi na sio kwa utaratibu huo mnaokwenda nao wa kukusanya majina ya walioomba na huenda mkuyapigia kura ni utaratibu mbovu kupita maelezo. Naamini TFF ina viongozi makini, wasomi na nzuri zaidi wapo waliocheza kwa upeo wa kimataifa, tangu mtemi Ramadhani wanao uwezo wa kujua hili pumba na huu ni mchele tunataka mchele hatutaki pumba, najua kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa ni mbaya zaidi, mnao uwezo wa kwenda kwa nchi nyinginezo kujua walifanyaje mchakato wa kumpata kocha na wanamlipaje na mambo mengi tu yanayohusu huyo kocha.
 
          Binafsi utaratibu wa kuomba nafasi ya ukocha kama kuomba nafasi za kazi mimi naushangaa watu wanaangalia kutokana na matakwa yao, juzi tu Nigeria walimtaka kocha wa timu ya Taifa ya Misri walidhani ndiye atakayeweza kuwafikisha mbali  katika kombe la dunia hawakuandika katika mtandao na kama sisi, bado nakaribisha maoni katika suala hili.  Je ni sahihi kumtafuat kocha wa Taifa stars kwa njia ya kutuma maombi? Mawazo ya wadau nayaheshima na nitayatumia
 
 
 
Asalam alyekum.
 
 
Mwandishi wa makala hii ni mfanyakazi wa mamlaka ya Bandari TPA kitengo cha uhandishi pia ni kocha mzoefu nchini.
 
Anapatikana Email     kennymwaisabula@yahoo.com 0713 – 243711
 
Championi yetu@gmail.com

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)