Translate in your language

Wednesday, March 17, 2010

Baada ya 'Lonely', mbioni kutoa 'HOPE'

 
EKSICUSIVE NEWS-BLOG  team
 

 
Mkurugenzi wa kampuni y Tang-Film,iliyotoa filamu kali iliyojaa udhuni na ukatili wa hali ya juu, ya 'Ilonely' , Sadique Bwanga, 'Alex  Damiani'  amesema yupo mbioni katika matayarisho kabambe ya kutoa filamu mpya nyingine itakayokwenda kwa jina la 'HOPE'.
 
Akizungunmza na 'Blog HII ' leo mapema leo, alisema kuwa, baada ya kuona filamu ya Lonely kupata shavu kwa Watanzania wengi ambao wanainunua filamu hiyo kwa kiasi kikubwa, na kuikubali kazi hiyo, ameona ni bora kutoa kitu kingine ili kuendelea kuwapa kitu bora.
 
"Tunawashukuru watanzania kwa sasa kwa jinsi walivyoipokea kazi yetu ya Lonely, ambayo ilikuuwa ndiyo ya kwanza, hivyo kwa kuipokea hivyo kwa sasa tupo mbioni kutoa filamu hiyo ambayo nayo itakuwa kali zaidi na  ambayo imejaa mambo ya mafunzo kwa jamii' alisem Bwanga.
 
Bwanga ambaye katika filamu hiyo ya Lonely aliigiza kama 'Alex Damiani' ambaye aliigiza kwa ubora wa hali ya juu ambapo alionyesha ukatili wa kutisha ambao tunaweza kusema unakaribiana na ukweli kwa kumchoma moto mtoto mchanga. ,,,, na yeye kuishia jera.
 
 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)