Translate in your language

Sunday, March 21, 2010

AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA MANILA

 

MKAZI wa Boko Basihaya, aliyefahamika kwa jina la Kimoro Ramadhan (35), amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya Manila aliyoifunga katika dirisha la chumba cha dada yake.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema tukio ilo lilitokea  jana majira ya saa 12 jioni katika eneo hilo la Boko, ambapo mtu huyo akiwa amepoteza maisha, akiwa ananing'inia katika dirisha hilo.

 

Kalinga alisema kuwa, sababu za kujinyonga kwake mtu huyo bado hazijafahamika mara moja kufuatia marehemu hakuacha ujumbe wowote na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi unaendelea.


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)