Translate in your language

Sunday, March 21, 2010

 

TWIGA STARS YAPATA AJALI

 

Na mmwablog wetu Dar

 

TIMU ya soka ya Wanawake ya Tanzania, 'Twiga Stars' jana  kilinusurika baada ya basi lao lililokuwa limewapakia kupata ajali na walipokuwa wakirejea katika kambi yao.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Eliasi Kalinga alisema kuwa timu hiyo iliopata ajali majira ya saa 12 45 jioni  katika eneo la Kigogo barabara ya Kawawa wakati wa timu hiyo ilipokuwa ikitoka uwanja wa Taifa ilipokuwa ikicheza na Ethiopia.

 

Katika tukio hilo, Kalinga alisema kuwa, gari lililokuwa na namba T285 ALH aina ya Fuso, likiendeshwa na Hashimu Ramadhan (45), katika eneo hilo la Kigogo 'round about' lilimshinda nguvu na kuligonga basi hilo la Twiga Stars lililokuwa na namba T 528 ASJ aina ya coastal, bus, ambalo likiemdeshwa na Hajj Mohammed.

 

Katika ajali hiyo, mmoja wa wachezaji wa Twiga, Mwanahamisi Omari(19) alijeruhiwa sehemu za mbavu pamoja na paji la uso,ambapo wengine walipata majeraha kidogo katika miili yao ambapo wote walikimbizwa katika Hospitali ya Tifa Muhimbili na kupatiwa matibabu na kuruhusiwa.

 

Hata hivyo leo alipo wasiliana na Mwanahamisi Omari "Gaucho" kujua hali yake, alisema kuwa anaendelea vizuri na yupo fiti. "Nashukuru naendelea vizuri Watanzania wazidi kutuombea ilitufanikiwe zaidi' alisema Mwanahamisi.

 

Jeshi hilo la Polisi linaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha ajali hiyo, kufuatia kukimbia baada ya kuligonga basi hilo. Kwa upande wa wadau wa soka nchini walisema kuwa hilo ni jambo la fedheha kwa timu ya Taifa ambayo inawakilisha nchi bila kuwa na ulinzi wa kutosha hadi kukumbwa na tatizo hilo.

 

Mwisho 

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)