Mkufunzi na mtafiti, Daktari John Odindi, kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini Afrika Kusini (kulia) katika mahojiano maalum na mwandishi wa Habari mwandamizi wa blog ya modewjiblog.com, Andrew Chale kwenye mkutano wa wanasayansi juu ya mabadiliko ya tabianchi, unaoendelea kwenye ukumbi wa Makao makuu ya UNESCO, Paris, Ufaransa (Picha na Mpiga picha maalum).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[Paris, Ufaransa] Watafiti kutoka chuo kikuu cha KwaZulu-Natal, Durban nchini Afrika Kusini wamewasilisha mada juu ya mabadiliko ya tabianchi kuhusiana na ongezeko la joto kwenye miji (urban temperature increase) ya Durban, East London na Port Elizabeth kwenye nchi hiyo.
Mada iliyowasilishwa na Daktari John Odindi katika mkutano mkubwa wa wanayasansi juu ya siku za usoni na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ‘Our Common Future Under Climate Change’ unaofanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa. Mkutano huo wa siku nne (Julai 7-10) unawajumuisha wanasayansi zaidi ya 2500 kutoka pembe zote duniani.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Dk. Odindi ambaye ni mkufunzi na mtafiti anasema hali ya ongezeko la joto ni kubwa na kupitia utafiti huo wanashauri jamii kuchukua hatua dhidi ya kukabiliana nayo.
“Utafiti wetu tuliowasilisha ni tumeangalia namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi dhidi ya joto katika miji hii kwani linakuwa kubwa kutokana na ongezeko la makazi mengi ya watu, viwanda na shughuli za kila siku za wananchi” alibainisha Dk. John Odindi.
Dk. John Odindi anashauri uhifadhi na utunzaji wa mazingira ya asili ikiwemo mimea, chemichemi za maji ya asili na mito kulindwa kwani vitu hivyo ndivyo vinavyosaidia kupunguza hali ya joto mijini.
Hivyo ansema kupitia mkutano huu wa Wanasayansi, kuelekea mkutano mkuu wa 21 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiriko ya Nchi (COP21) utakaofanyika Paris , Desemba mwaka huu, anatumai kwamba mataifa yatajumuika kutafuta muafaka za kupunguza kiwango cha joto duniani.
Pia anabainisha kuwa, nchi ya Afrika Kusini imejidhatiti katika kukabiliana na hali hiyo ya tabianchi katika ongezeko la joto mijini kwani mkutano wa COP17, ulifanyika katika jiji la Durban, Afrika Kusini.
Mada hiyo inaenda sanjari na matakwa ya mataifa mbalimbali juu ya kukabiliana na kiwango cha hali ya joto na nyuzi mbili (to reduce temperature level by 2 degrees).
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa