UMUHIMU
WA KUSHIRIKISHA JAMII KATIKA UIMARISHAJI WA AFYA NA USAFI KATIKA MAENEO YAO
Eneo la mafunzo:
Lugono, wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro
Imeandaliwa na Othman
R. Masanga kutoka QI presentation kuchimba dawa katika kikao cha tatu cha
kuboresha huduma za afya Tanzania, tarehe 27 novemba 2013, Mlimani conf centre
Tatizo la
maeneo/vituo yanayotumika na abiria kwa kushuka na kupata mahitaji yao, kwa
mfano:- kujisaidia (kuchimba dawa), vyakula na huduma za simu limekuwa tatizo
na kukua siku hadi siku.
Tanzania bara ina
sehemu/vituo vingi kwa abiria, wafanyakazi na waendesha magari makubwa ya
mizigo na mabasi kusimama na kupata mahitaji yao pembezoni mwa barabara kubwa
ziendazo mikoani, sehemu zisizo na maeneo, vifaa na faragha kwa ajili ya
kujisaidia na kupelekea uchafuzi wa mazingira wa maeneo husika na usambaaji wa
magonjwa kwa wasafiri na wenyeji kwa ujumla.
Lugono ni moja ya
sehemu inayotumika kwa wasafiri kupata mahitaji yao kama kuchimba dawa na
vyakula, ipo umbali wa kilomita 25 toka morogoro mjini na kulingana na taarifa
za mkoa wa morogoro mwaka 2010 eneo hilo lilikumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu, lakini pia eneo limekuwa na hatari kwa wasafiri kugongwa na nyoka
kwasababu watu walikuwa wakiingia porini na vichakani kutafuta usiri wakati
wakijisaidia.
Kwa kuona tatizo
ofisi ya afya mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na wadau wengine waliona
umuhimu na kufanya yafuatayo:-
Njia zilizotumika:-
katika picha hapo juu ni viongozi katika nyadhifa zao wakiwa katika mikutano ya kuhamasisha jamii kushiriki kwa pamoja kukabiliana na tatizo lililo mbele yao
Hali iliyokuwepo kabla ya ukamilishaji wa mpango huo
kama inavyoonekana katika picha:-
![]() |
| wanafunzi wakipata mahitaji ya vyakula walipokuwa katika ziara yao kwenda mikumi kuangalia wanyama pori huku kukiwa na lundo la taka karibu na eneo la vyakula |
![]() |
| vyakula vikiandaliwa katika mazingira machafu ambayo ni chanzo cha magonjwa ya matumbo kwa walaji |
![]() |
waandaaji wa nyama choma wakiwa hawana sare za
kazi
|
Matokeo baada ya uhamasishaji:
Jamii ilichangia milioni ishirini (TShs 20,000,000/=) kwa kuuza mifugo
na mazao kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika eneo hilo. Vyoo vilijengwa kwa awamu mbili tofauti, choo
cha kwanza kikiwa na vyumba 14 vya kujisaidia na baada ya mwaka kilijengwa kingine
chenye idadi ya kama hio
![]() |
| ) Eneo la nje la jengo la choo bora |
![]() |
| Eneo la ndani la choo cha awamu ya pili kikiendelea na ujenzi |
![]() |
Matunda
yakiwa yamepangwa juu ya vichanja na utunzaji mzuri wa takataka katika ndoo za
plastiki
|
![]() |
| Kundi la vijana waliojiajiri wakiwa na sare zilizopendeza na safi |
![]() |
| Afisa mifugo akikagua nyama kabla ya kuthibitishwa kuwa salama kwa matumizi ya binadamu |
![]() |
| Nyama iliyokutwa na vimelea vya ugonjwa wa TB |
![]() |
Wasafiri wakipata mlo katika mazingira safi na salama
|
![]() |
| Eneo la kunawia mikono ikiwa na sabuni ya maji |
Changamoto zinazojitokeza:-














No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa