Akizungumza jijini Dar es salaam, Mratibu wa onyesho hilo la pamoja Dar Modern na Nadd Ikhwan Safaa (Malindi ya Zanzibar), Bakari Hassan alisema hilo la Usiku wa Mwambao Asilia, litaenda sambamba na kuwapongeza mashabiki wa soka wa Azam Fc waliotwaa ubingwa huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza 2013/2014.
“Usiku wa Mwambao asilia, Aprili 19, pale Travertine utakuwa na shamrashamra mbali mbali ikiwemo za kuwapongeza Azam na mashabiki wao watakaofika kwenye onyesho hilo maalum” alisema Bakari.
Kwa upande wake, Mlezi wa Heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema usiku huo pia utakuwa ni maalum ikiwemo pia kuwakutanisha magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, ambao wataimba nyimbo za zamani na za sasa.
“Kwa kiingilio cha sh 10,000 tu, usiku huo utapambwa na ‘surprise’, mbalimbali kwa wadau kupita kwenye zuria jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria usiku huo” alisema Asia Idarous.
Aidha, Asia, alisema tayari tiketi za onyesho hilo zimeshaanza kuuzwa sehemu mbalimbali ikiwemo duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda. Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa