Translate in your language

Friday, March 28, 2014

KENYA NA RASIMU YA WAKE WENGI


Ancentus (Danger) okuku akionekana pichani mwaka 1984, ni mkenya anayesemekana kuwahi kuwa na wake wengi zaidi, inasadikiwa kuwa na wake zaidi ya 100 katika kipindi cha maisha yake
wakati vuta na kuvuta ikiendelea katika Bunge la Kenya juu ya mswada unaopendekeza mwanaume kutoomba ridhaa kwa mke wake wa kwanza pindi atakapohitaji kuongeza mke wa pili au watatu nk

wabunge wengi wanawake wamepinga, mwanaume kuoa bila ya kuomba ridhaa kwa mke wa kwanza na kupendekeza kuwepo na kibali maalum toka kwa mke wa kwanza kwa kumruhusu mume wake kuongeza mke. 

Wakati  wabunge wa kiume wamesikitishwa na pendekezo hilo toka kwa wabunge wanawake, wakisema kuwa ndoa zote za kimila za kiafrika mwanamke pindi anapokubali kuolewa, huwa tayari ameshakubaliana kuwa na mitala kwa maana ya  mume wake kuwa na wake zaidi ya mmoja, hivyo kupendekeza mwanaume kuomba kibali kwa mke wa kwanza ni kinyume cha maadili ya mwafrika

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)