Dodoma. Huku wajumbe wakitaka kura za kumchagua mwenyekiti Bunge Maalum la Katiba zipigwe kwa siri, tayari baadhi ya majina ya wakongwe wa siasa Tanzania yameshaanza kutajwa kuwa na sifa za kukamata ofisi hii nyeti.
Miongoni mwa wanaotajwa kuwa na sifa ya kushika wadhifa huo ni Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samwel Sitta.
Sitta anaheshimika kwa uwezo wake wa kuliendesha bunge la Jamhuri kwa spidi na kwa ufanisi mkubwa. Wakati wa uongozi wake, Watanzania walishuhudia wabunge wakifichua kashfa mbalimbali za ufisadi ikiwemo Richmond.
Mwingine anayetajwa kuwa anafaa kuwa mwenyekiti ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Serikali ya Awamu ya Tatu.
Kwa mujibu wa rasimu ya kanuni za uchaguzi zilizosambazwa kwa wajumbe jana, endapo kutakuwa na mgombea mmoja tu, basi mgombea huyo atapigiwa kura ya ndio ama hapana.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa