Translate in your language

Thursday, January 9, 2014

Mawaziri wa ulinzi na wa mambo ya ndani kutoka nchi za Uganda,Rwanda na Kenya wametia saini makubaliano kuweka himaya moja ya ulinzi miongoni mwa nchi hizo.

Hii ni mara ya kwanza kuwepo kwa mkataba huo na hii ina maana nchi moja ikipata matatizo ya usalama nchi nyingine zitakuwa na uhuru wa kuingilia kati na kusaidia. Kikao cha mawaziri hao kilitanguliwa na kile cha wakuu wa majeshi na polisi kutoka nchi hizo ambacho pia kilitathmini changamoto za kiusalama kwenye eneo hilo na jinsi ya kuimarisha ushirikiano miongoni mwa mataifa hayo

chanzo: idhaa ya kiswahili ujerumani (DW), kusikiliza taarifa kamili bonyeza hapa


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)