MAHMOUD THABIT KOMBO KUUNGURUMA LEO UWAMJA WA BUSTANINI
Na Andrew Chale, Zanzibar
CHAMA cha Mapinduzi CCM, leo Januari 28, kinatarajia kufanya kampeni yake ya Sita (6) ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la uwanja wa Bustanini, katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki, ambapo mgeni rasmi wa kumnadi Mgombea anatarajiwa kuwa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi wa CCM, Mohammed Yusufu Mrefu.
Akielezea mkutano huo wa Sita wa hadhara, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi jioni, eneo hilo la Bustanini, Mahmod Thabit Kombo , aliwaomba wananchi wa wa Kiembesamaki kufika kwa wingi kwenye mkutano huo, ambapo pia kutakuwa na shamrashamra mbalimbali zitakazoanza majira ya Saa Nane, mchana. Hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.
"Leo Januari 28, nawaomba wananchi wa Kiembesamaki, kujitokeza kwa wingi eneo la Bustanini.. ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya chama" alisema Mahmoud Thabit Kombo.
Aidha, aliwaomba wananchi wa Jimbo hilo, ifikapo Februari 2, 2014 siku ya Jumapili, kumpa kura za NDIYO, ili awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea Bungeni kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.
Baadhi ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia siku ya leo kwenye mkutano huo ikiwemo kero za maji, elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la Kiembesamaki, pindi watakapomchagua kuwa mwakilishi wao.
Mwisho
Picha mgeni rasmi Yusuf Mrefu
na Picha za Mahmoud Thabit kombo
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa