MAHMOUD THABIT KOMBO
KUUNGURUMA LEO KWENYE MKUTANO WA HADHARA –BUYU PWANI
Na Andrew Chale, Zanzibar


Akielezea mkutano huo wa tatu wa hadhara, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi jioni, eneo hilo la Buyu- Chukwani, Mahmod Thabit Kombo , aliwaomba wananchi wa Buyu kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.
"Leo Januari 24, nawaomba wananchi wa Buyu, kujitokeza kwa wingi ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya chama" alisema Mahmoud Thabit Kombo.
Aidha, aliwaomba wananchi wa Buyu, ifikapo Februari Mbili, siku ya Jumapili, wampigie kura ya NDIYO, ilki awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.
Baadhi ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia ikiwemo kero za maji, elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la Kiembesamaki, pindi watakapomchagua.
Mwisho
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa