Translate in your language

Saturday, December 21, 2013

Baraza la Usalama la UN, laitisha mkutano wa dharura kuhusu Sudan Kusin

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao cha dharura hivi leo chenye lengo la kudhibiti vitendo vya umwagikaji damu vinavyoendelea nchini Sudan ya Kusini.


Wakimbizi katika eneo la Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika mauwaji
Ripoti za hivi punde zikisema wanajeshi wa Uganda wameshapelekwa katika mji mkuu wa Juba.Yote yanajiri baada ya kuuwawa walinzi watatu wa amani wa Umoja wa Mataifa kutoka India. Ikiwa si zaidi ya miaka mitatu tangu kuundwa kwake taifa hilo changa kabisa duniani, tayari mapigano yanayoonekana kama yanafanyika kwa misingi ya kikabilia yameshasababisha vifo vya mamia ya watu wakiwemo walinzi watatu wa amani wa Umoja wa Mataifa.
Awali jana, kundi la vijana wenye silaha walivamia maeneo ya Umoja wa Mataifa mjini Jonglei na kuwajeruhi watu kadhaa. Katika hatua nyingine baadaye wanamgambo kama hao waliwalenga na kuwauwa wanajeshi watatu kutoka India.
Taarifa ya mwakilishi wa India katika Umoja wa Mataifa
UN-Sicherheitsrat Resolution zu Syrien Chemiewaffen 27.09.2013
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
Balozi wa India katika Umoja wa Mataifa, Asoke Mukerji, alithibitisha kutokea mkasa huo nchini Sudan ya Kusini mbele ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Huu ni mkasa wa kwanza wa mauwaji ya wahudumu wa Umoja wa Mataifa katika mapigano ya taifa hilo. Katika kikao cha jana jioni Balozi wa Pakistan katika umoja huo Masood Khan aliomba wajumbe wa mkutano wakae kimya kwa dakika moja ikiwa ishara ya kuwakumbuka waliowawa nchini Sudan ya Kusini.
Baraza hilo lilipanga kuanza mkutano wake wenye lengo la kujadili machafuko yanayoendelea katika taifa hilo asubuhi ya leo. Ndani ya Sudan na hasa katika mji wa Juba kazi ya dharura ya kuwanusuru raia ya wa kigeni wanaoishi nchini humo imeanza. Ndege na helkopta zimekuwa zikiwachukua raia wa Marekani, Uingereza, wafanyakazi wa mashirika ya misaada pamoja na Maafisa wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuwanusuru na vurugu.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)