|
Mh. Zitto Kabwe |
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameonekana kuwa tisho kubwa ndani ya Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tishio la Zitto, lilionekana wazi jana, wakati wa uchaguzi wa kuwapata wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, baada ya kumbwaga Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo tangu mwaka 2005.
Katika uchaguzi huo, ulioongozwa na kanuni za Bunge, Zitto aliibuka na ushindi wa kura 13 dhidi ya 4 za Cheyo, kati ya kura 17 za wajumbe.
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa PAC kwa kuibuka na ushindi wa kishindo wa kura 13 na kumshinda mpinzani wake, Zainabu Vullu, ambaye aliambulia kura 4.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa