HUJUMA dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), zinazidi kulitikisa kutokana na kuibuka kwa wimbi jipya la wizi wa nyaya katika nguzo za msongo mkubwa wa umeme mkoani Kilimanjaro.
Uchunguzi wa gazeti hili uliothibitishwa na Tanesco, umebainisha kipindi cha Januari mwaka jana hadi Januari 2013, nyaya zenye urefu wa mita 6,650 zenye thamani ya Sh100 milioni zimeibwa.
Licha ya kuibwa kwa nyaya hizo zenye Copper, Transfoma10 zilihujumiwa kwa kipindi hicho na kulisababishia shirika hilo mkoani Kilimanjaro hasara ya Sh50 milioni. Vyanzo mbalimbali vimedokeza kuwa wizi huo ambao hupangwa kwa ustadi mkubwa, hufanywa na ama mafundi uchwara (Vishoka) au baadhi ya waliowahi kuwa watumishi wa shirika hilo.
“Hakuna mtu wa kawaida anaweza kupanda nguzo zile za umeme wa njia kubwa. Kwanza anapandaje maana kuna vifaa vyake ni hatari sana lazima wawe wataalamu,” alihoji mkazi mmoja wa Moshi.
Uchunguzi zaidi umebaini kwa Desemba pekee, kulikuwapo matukio matano ya kuibwa kwa nyaya hizo eneo la Shirimatunda na matukio yote yalitokea kati ya saa 7:30 na saa 9:00 usiku.
Kuibwa kwa nyaya hizo kulisababisha kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo kama Soweto, Shanty Town, Mailisita na Machame na Tanesco kufanikiwa kurudisha umeme baada ya saa 12 kupita.
Soko kuu la waya za Copper Ofisa kutoka taasisi moja nyeti ya Serikali, alidokeza kuwa nyaya hizo zinazoibwa zimekuwa zikisafirishwa kupitia njia za panya hadi Mombasa nchini Kenya.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa