| |
|
Matukio Duniani | |
|
Ndege za Urusi zaelekea Syria |
|
Ndege mbili za wizara ya masuala ya dharura nchini Urusi, zilizobeba msaada wa kibinaadamu leo zimeelekea katika mji wa Latakia, Syria. |
|
Pistorius afikishwa mahakamani mara ya pili |
|
Wakili anayemtetea bingwa wa michezo ya Olimpiki ya walemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, amesema mauaji yaliyofanywa na mwanariadha huyo yalikuwa ya bahati mbaya. |
|
Mkutano kuhusu Mali kufanyika Mei |
|
Umoja wa Ulaya umeandaa mkutano wa kimataifa wa kusaidia kuijenga upya Mali, utakaofanyika mwezi Mei, mwaka huu. |
|
ICC kuamua hatma ya Gbagbo |
|
Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC, leo wataamua iwapo kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo, ya kuhusika na ghasia ya baada ya uchaguzi nchini mwake, miaka miwili iliyopita. |
|
Chavez apelekwa hospitali Caracas |
|
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, amepelekwa katika hospitali ya jeshi mjini Caracas baada ya kurejea nchini humo jana usiku, akitokea Cuba. |
|
Jebali kukutana na Rais Marzouki Tunisia |
|
Waziri Mkuu wa Tunisia, Hamadi Jebali, amesema leo atakutana na rais wa nchi hiyo, Moncef Marzouki, kutafuta suluhisho baada ya jitihada za kuunda serikali ya wasomi wasio wanasiasa kushindikana. |
|
Rais wa Armenia ashinda uchaguzi |
|
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa jana nchini Armenia, yanaonyesha kuwa rais aliyeko madarakani, Serge Sarkisian, ameshinda katika uchaguzi huo. |
|
| |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa