Nafaham ni watanzania wengi
ambao wanalo hili swali kama mimi, toka tulipoacha kumuona
msanii/mchekeshaji Vengu kwenye ORIJINO KOMEDI baada ya kuumwa, zilizuka
stori nyingi sana lakini stori ya mwisho mimi kuipata ni kwamba
alisharudi Tanzania akitokea kwenye matibabu India na afya yake
inaendelea vizuri.
Baada ya kufahamu hivyo nikawa
na kiu ya kutaka kujua ni lini tutaanza kumuona akichekesha tena ndani
ya Orijino Komedi hivyo nikapata nafasi ya kuzungumza na Wakuvanga ambae
ndio mkurugenzi wa kampuni inayoisimamia Orijino Komedi.
Namkariri akisema “ukweli niwe
muwazi, kwa afya yake na tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa
wa fahamu, tunazungumzia kitu kinaitwa ubongo, hayo matatizo yanachukua
muda mrefu sana ukizungumza ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi
karibuni unakua unajidanganya wewe na watanzania wenzio, ndio maana siku
zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea mtu unaempenda muombee, mi
siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au mwaka ujao”
Kuhusu kutafuta mtu wa kuziba
nafasi ya Vengu, Wakuvanga amesema “tutaendelea kuwa na jina la Vengu
maisha yote ya Komedi, kwetu sisi iko tofauti kidogo sisi tumeapa..
ndivyo tunavyoishi, tuko saba mpaka tunakufa.. kuongezeka kwa mtu labda
sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini tutaendelea kuwa saba,
hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi tunaishi tuko
saba, akipungua mmoja bado tuko saba”
source:http://millardayo.com/
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa