Daudi Mwangosi enzi za uhai wake |
Uongozi wa Africa Media, ambao ni wamiliki wa kituo cha televisheni "Channel 10" Tanzania umelaani vikali mauwaji ya mwandishi wake Daudi Mwangosi.
Mwangosi aliuwawa kutokana na mripuko wa bomu wakati wa purukushani za polisi na wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA zlizotokea katika ufunguzi wa matawi ya chama huko Mkoani Iringa
Daud Mwangosi ameuwawa jana katika vurugu za Polisi na wafuasi wa CHADEMA katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa.
Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za CHADEMA Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.
Kabla ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Askari polisi akiwa na jeraha la risasi akiwa karibu na mabaki ya mwili wa mwandishi huyo |
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.
Mabaki ya mwili wa marehemu Daudi Mwangosi ukiwa umeharibika kutokana na mlipuko huo |
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa CHADEMA kurushiana mawe kwa mabomu, zaidi ya magari matano ya CHADEMA na ya wananchi yameharibiwa, huku watu kadhaa wakiachwa wamejeruhiwa hadi kupelekea mwanahabari mmoja, Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa