Translate in your language
Wednesday, August 8, 2012
Uganda: Mkutano wa Kimataifa kutoka kanda ya maziwa makuu wafanyika Kampala
Mkutano wa Kimataifa wa viongozi wa Afrika kutoka kanda ya maziwa makuu umeanza leo jijini Kampala, Uganda.
Mkutano huo utajadili kwa kina mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na namna ya kupata suluhu juu ya mzozo huo, ikiwemo kuundwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani na kupambana na waasi wa M23 wanaoyumbisha amani ya DRC.
Mkutano huo unajumuisha nchi 11, zikiwemo Angola, Burundi, Congo, Kenya, Rwanda, Sudan,Tanzania, Zambia na mwenyeji, Uganda.
ukitaka kusikia kwa sauti habari hii bonyeza hapa
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa