Martin Shikuku enzi za uhai wake |
Kenya inaomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe MartinShikuku aliyefariki hapo jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya saratani.
Shikuku amefariki akiwa na umri wa miaka 79 akipokea matibabu katika Hospitali ya Hurlingham Nairobi.Shikuku alikuwa mbunge wa eneo la Butere Magharibi mwa Kenya hadi mwaka 1997,lakini harakati zake katika mapambano ya kupigania Uhuru ni jambo ambalo halitosahaulika katika fikra za Wakenya.
Saumu Mwasimba amezungumza na Aliyekuwa makamu wa rais wa Kenya bwana Moody Awori ambaye ametoka mbali kisiasa pamoja na mwanasiasa huyo mkongwe.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa