Translate in your language

Saturday, February 18, 2012

Wanafunzi wanane wadaiwa kumbaka mwalimu kwa zamu

kutoka gazeti la mwananchi,
WANAFUNZI wanane wa Shule ya Sekondari Bagamoyo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo kujibu tuhuma za kumbaka mwalimu wao kwa zamu.

Katika kesi hiyo iliyojaza umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo, imedaiwa kuwa wanafunzi hao walimbaka mwalimu huyo kwa zamu na kumsababishia maumivu makali.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, William Mwantela alimwambia Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa kuwa wanafunzi hao walitenda kosa hilo Januari 16 mwaka huu katika mazingira ya shule hiyo.

Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Emmanuel Antoni, Fadhili Nassoro, Nassa Yohana, Benjamini Mhina, Yusuph Timothy, Frank Jackson, Frank Kanya na Hamisi Timbwa.

Mwendesha mashtaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa tukio hilo lilitokea shuleni hapo Januari 16 mwaka huu majira ya saa 9:00 jioni.

Hata hivyo, watuhumiwa hao wote walikana shtaka na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 29 mwaka huu baada ya mwendesha mashtaka huyo kudai kuwa ushahidi haujakamilika.

Awali kabla ya kuahirisha kesi hiyo upande wa utetezi ulimwomba hakimu kuruhusu dhamana na hakimu aliruhusu akitaka kila mmoja adhaminiwe na mtu mmoja mwenye hati na kitambulisho ambaye atasaini hati ya dhamana ya Sh2milioni.

Washitakiwa watatu walifanikiwa kutimiza masharti hayo ya dhamana na wako nje, lakini wengine watatano wameshindwa na kupelekwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena siku iliyopangwa.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)