UTAFITI: WANAUME WENGI BADO WANAPEWA KICHAPO NA WAKE ZAO KENYA!
Siku ya Leo ya wapendanao duniani ambayo wengi huitumia kuenzi mapenzi yao, huko kenya imethibitika kwamba baadhi ya wanaume hawaisherekei kwasababu ya maumivu waliyonayo ya kupigwa na kunyanyaswa na wake zao.
mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini humo Nderitu Njogu, amesema idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka sana ambapo utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwafanya wawadharau wanaume.
Nderitu amesema sababu nyingine kubwa ya wanawake kuwanyanyasa wanaume ni uwezo mkubwa wa kifedha walionao wanawake kuliko waume zao ambapo hii ishu imeripotiwa na BBC leo, wakati wiki iliyopita Polisi walimkamata na kumuweka ndani mwanamke mmoja mjini Nyeri huko mkoa wa kati, baada ya kumshambulia mume wake na kumjeruhi vibaya kwa panga ambae kwa sasa bado kalazwa hospitali, yani huyo mwanaume.
Kwa kumalizia, Bw Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume laki nne na elfu sitini, walinyanyaswa na wake zao mwaka jana ambapo utafiti wa shirika lake unaonyesha kesi nyingi za waume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika mkoa wa kati
.
.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa