Na Peter Mwenda, Igunga
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewataka wananchi wa Igunga kutokipigia kura Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa
kuwa si chama cha kitaifa na hakijakomaa kisiasa.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohamed, wakati akimnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Bw. Leopold Mahona katika viwanja vya Barafu mjini hapa.
Mbunge aliwahi kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni kabla ya Bw. Freeman Mbowe wa CHADEMA kuchukua nafasi hiyo, alidai kuwa chama hicho hakijakomaa kisiasa ndiyo maana kinajihusisha na vitendo vya vurugu ikiwemo kumwaga tindikali, kupiga risasi na mengine na kwamba hiyo inaonesha hakiwezi kuleta maendeleo ya wananchi.
Alisema chama hicho kina ubinafsi, ndiyo maana kilijitenga bungeni na kuunda umoja wa wabunge wa CHADEMA peke yao tofauti na wakati alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo alishirikisha wabunge wa vyama vyote vya upinzani wakiwemo wa chama hicho bila ubaguzi.
Alidai sera za CHADEMA hazina tofauti za CCM ambao wanagawa madaraka kwa watoto wao, ndugu na jamaa badala ya kufuata utaratibu wa uongozi katika jamii.
Bw. Rashid aliyewasili mjini hapa juzi na helkopta ya CUF kujumuika na wabunge wengine wa chama hicho hivyo kufanya idaid yao kufikia 20, alisema chama chake ni cha kitaifa ambacho kina viongozi pande zote za muungano.
“Makamu wa Rais Zanzibar ni Katibu Mkuu wa CUF, sisi wabunge wa Zanzibar tumekuja kwa gharama zetu kumsaidia mwenzetu aingie bungeni kuwakomboa watu wa Igunga, niambieni CHADEMA kuna kiongoi gani Zanzibar,” alihoji Bw. Rashid.
Alisema wananchi wa Igunga wakitaka maendeleo ya kweli wamchague, Bw. Mahona kuwa mbunge kwa kuwa wana kila sababu ya kufanya hivyo ili kubadilisha maisha yao.
Naye Meneja Kampeni wa mgombea wa CUF, Bw. Antony Kayange, alisema wapiga kura wasipoteze muda kukipigia kura CCM kuwa wanakumbuka kumleta Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli kuwaongopea.
Alisema anawadaganya kujenga daraja la mto Mbutu ambalo limeahidiwa kujengwa miaka mingi iliyopita bila ahadi hiyo kutimizwa.
“Huyu Magufuli amekuwa madarakani kwa miaka 11 mbona hata siku moja hakufikiria kuja Igunga angalau kuona kero za wananchi, leo anakuja kudanganya kujenga daraja la Mbutu huo ni uongo, msikubali kurubuniwa kupigia kura CCM,” alisema Bw. Kayange.
Naye Naibu Katibu wa CUF Tanzania Visiwani, Bw. Ismail Jussa, alisema wananchi wa Igunga wasikubali kudanganywa na vyama vingine kwa kuwa wataendelea kukabiliana na matatizo waliyonayo bila kupata ufumbuzi.
Alisema katika majimbo ambayo CUF inaongoza yana maendeleo makubwa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kujenga hoja za wananchi na kuziwasilisha serikalini kufanyiwa kazi.
Mgombea ubunge Bw. Mahona akiomba kura kwa wananchi alisema kamwe hatakimbia jimbo lake kama wanavyofanya wabunge wengine bali atatumia muda wake mwingi kuwatumikia wananchi wa Igunga
1 comment :
Very good info. Lucky me I found your blog by chance (stumbleupon).
I've book marked it for later!
Feel free to visit my homepage - Different kinds of gynecomastia
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa