Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Bwana Yusuf Mahmoud ‘DJ Yusuf’ amebainisha kuwa, watu wengi wamekuwa na shahuku kubwa ya kuliona tamasha hilo hivyo kwa mwaka huu watalifurahia kwa kiwango kikubwa litakapolindika ndani ya viunga vya Unguja, Zanzibar.
“Watu wa rangi na umri tofauti kwa mara nyingine tena wataungana, kusherehekea muziki wa Afrika. Zanzibar itakuwa kwenye shamrashamara na mikusanyiko mikubwa ya wageni mbalimbali na mahoteli na maeneo mengine ya malazi na vyakula pamoja na sehemu za biashara zitaendelea kujaa maradufu” amesema Mkurugenzi wa tamasha hilo Yusuf Mahmoud.
Na kuongeza kuwa, kauli mbiu ya tamasha hilo kwa mwaka huu ni #AfricaUnited. Ikiwa na maana kuwa Muziki unaunganisha : Mtu na mtu, moyo na moyo. Katika dunia inayozidi kugawanyika, lugha ya muziki unaohamasisha umoja na urafiki na mshikamano kwenye mipaka yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud ‘DJ Yusuf’ akionesha kitabu chenye progamu ya tamasha hilo kwa mwaka huu wa 2017 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Sauti za Busara, Mh. Simai Mohamed Said amewashukuru wadau wote kwa kuendelea kuliunga mkono tamasha hilo kwani uwepo wake umesaidia na linaendelea kusaidia fursa za kiuchumi na kuinua tamaduni za kiafrika Duniani kote.“Tunaishukuru Serikali, Mabalozi, wadhamini wote, Wanahabari na wadau wenginekwapamoja kwa kuendelea kutuunga mkono na kufanikisha tamasha hili kubwa kabisa barani Afrika ambalo ni la 7 kwa ukubwa. Kwa ukubwa huo lakini tunapata changamoto hasa kwa kuwapata wafanyabiashara kujitokeza kuwekeza kwa tamasha letu kwani licha ya kuwanufaisha wafanyabiashara hao lakini wamekuwa nyuma sana kujitokeza kudhamini tunatoa wito kujitokeza na milango ipo wazi.
Mh. Simai Mohamed Said pia amebainisha kuwa, ametoa maombi rasmi kwa Serikali hasa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli akipata nafasi aweze kutembelea Zanzibar kujionea tamasha hilo kubwa kabisa Barani Afrika la Sauti za Busara.
“Napeleka maombi yangu rasmi kwa Rais wetu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, kumuomba akipata nafasi basi aje kujionea mwenyewe jinsi gani vijana, wananchi wake tunavyoitangaza Tanzania ili kutambulika katika mipaka tofauti na kuvutia fursa za kiuchumi, utamaduni na kiuwekezaji kwani pia tumekuwa tukipokea mabalozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani kote kuja kwenye tamasha hili na wawekezaji ambao wanafika Visiwani Zanzibar.” Amebainisha Mh. Simai Mohamed Said.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Sauti za Busara, Mh. Simai Mohamed Said akizungumza katika mkutano huo na wanahabari Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa tamsha hilo Dj Yusuf Mahmoud na mwisho ni Meneja wa tamasha, Journey Ramadhan
Naye Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mh. Hanne Marie Kaarstad ambao ni wadhamini wakuu na wa muda mrefu wa tamasha hilo wamepongeza juhudi za uongozi wa Sauti za Busara za kuinua utamaduniwa Mtanzania, Mzanzibar pamoja na tamaduni za Kiafrika kwa kupitia sanaa za muziki unaowakutanisha watu wote pamoja na kufurahia ala hizo za muziki ambapo pia amebainisha kuwa wataendelea kutoa sapoti kwa tamasha hilo.Kwa upande wake, Meneja wa tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan amesema kuwa, wasanii wote watatumbuiza ‘Live’ kwa asilimia 100 na hali hiyo hufanya tamasha hilo kuwala kipekee na tofauti kwani uonyesha uhalisia na ufanisi huku kipaumbele kikitolewa kwa wasanii chipukizi wanaofanya muziki unaotambulisha utamaduni.
Journey Ramadhan amebainisha kuwa,kipaumbele cha tamasha hilo ni kuhakikisha kila mmoja anamudu kiingilio hivyo kwa watanzania wataweza kulipia TSh. 6,000 kwa siku huku kwa atakayetaka kulipia kwa siku zote nne atalipa Tsh. 20,000.
Meneja wa tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan akizungumza katika tamasha hilo leo
Baadhi ya wasanii hao na makundo yao ni pamoja na : Freshlyground (Afrika Kusini), Rocky Dawuni (Ghana),Sarabi (Kenya), Pat Thomas & Kwashibu Area Band (Ghana), Simba & Milton Gulli (Msumbiji), Jagwa Music (Tanzania),Bob Maghreb (Morocco), Karyna Gomes (Guinea Bissau) na Sami Dan and Zewd Band (Ethiopia), Chibite Zawose Family (Tanzania).
Wengine ni Rajab Suleiman & Kithara (Zanzibar), Wahapahapa Band (Tanzania), Buganda Music Ensemble (Uganda), Batimbo Percussion Magique (Burundi), Kyekyeku (Ghana), H_art the Band (Kenya),Grace Barbe (Seychelles), Roland Tchakounté (Cameroon / France), Imena Cultural Troupe (Rwanda), Isau Meneses (Mozambique).
Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo hiyo Februari mwaka huu
Pia wapo Jessica Mbangeni (South Africa), Sahra Halgan Trio (Somaliland), Tausi Women’s Taarab (Zanzibar), CAC Fusion (Tanzania), Ze Spirits Band (Tanzania), Loryzine (Reunion), Madalitso Band (Malawi), Mswanu Gogo Vibes (Tanzania), G Clef Taarab Orchestra (Zanzibar), Afrijam Band (Tanzania)Wengine ni Cocodo African Music Band (Tanzania), Kiumbizi (Pemba / Zanzibar), Rico and the Band (Zanzibar), Usambara Sanaa Group (Tanzania), Mcharuko Band (Zanzibar) na Taarab – Kidumbak Group na wengine wengi.
Tazama MO tv kuona tukio hapa:
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mh. Hanne Marie Kaarstad akizungumza katika tukio hilo
Wanahabari wakifuatilia tukio wakati wa mkutano huo wa Sauti za Busara mapema leo 24 Januari 2017
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Sauti za Busara, Mh. Simai Mohamed Said akijibu baadhi ya maswali wakati wa mkutano huo. kulia ni Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mh. Hanne Marie Kaarstad
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiuliza maswali katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog, Bw. John Bukuku akiuliza swali katika mkutano huo, kulia kwake ni Salome George aliyekuwa akisimamia zoezi hilo kwa waandishi wa Habari
Mkutano huo ukiendelea
Mwenyekiti wa Bodi ya Tamasha la Sauti za Busara, Mh. Simai Mohamed Said akizungumza katika mkutano huo na wanahabari Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani). Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa tamsha hilo Dj Yusuf Mahmoud na mwisho ni Meneja wa tamasha, Journey Ramadhan. Kulia ni Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mh. Hanne Marie Kaarstad. (Habari, Picha na Andrew Chale)
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa