Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la ufungaji wa sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Akitoa hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.
Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.
“Uwepo wenu tunaupongeza kwani naamini mumekuwa mstari wa mbele katika kuliombea Amani Taifa hili na pia kuwaombea ulinzi watu mbalimbali pamoja na kutoa misaada, huduma za Afya na mambo mengine mbalimbali. Hii ni faraja sana na Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.
Aidha, katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wote.
Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo ikiwemo suala la ushoga.
“Serikali haipo tayari kuona vitendo vya ushoga vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangaza kwa jamii. Wizara yangu itakutana na NGOs, zote za Kijamii na taasisi zilizosajiliwa ambazo pia zingine zipo chini ya Wizara yetu kukaa nazo na kujua ni zipi zinajihusisha na masuala haya iwe kwa kutetea ushoga ama kubariki vitendo hivi, tutawachukulia hatua kali za kisheria na hata kuzifuta kabisa” alimalizia Dk. Kigwangalla.
Aidha, katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango vyake..






Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilika
Muonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa




Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi


Matembezi ya sherehe hiyo yakiendelea

Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50

Vikundi vya matembezi yakiendelea



Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua gwaride la vijana hao



Vijana PF wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi (Hayupo pichani)




Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo



Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo





Mzee Boman ni miongoni mwa Wazee waanzilishi wa kanisa hilo ambalo kwa sasa limetimiza Jubilee ya Miaka 50.

No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa