Translate in your language

Friday, July 22, 2016

AMANA BANK TANZANIA WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

Juma Msabaha ambaye ni senior costomer service manager wa Bank Ya AMANA nchini Tanzania akifafanua jambo kwa wanahabari wakati Bank Hiyo ikizindua Rasmi Kituo cha Huduma kwa wateja ambacho ni mahsusi kwa kuwasaidia wateja wake kuzifikia na kuzipata Huduma Zao kiurahisi zaidi



Benki ya kwanza ya Kiislam nchini Tanzania Amana benki leo imezindua kituo chake cha huduma kwa wateja
ambacho kitakuwa kikiwasaidia wateja wake kuweza kupata taarifa mbalimbali 
kuhusu huduma zao kama maulizo kuhusu bidhaa za amana, Atms,huduma za mitandao (simu 
banking) na amana banki mtaani n.k.


Kituo hicho kitakuwa kikifanya kazi kuanzia saa 2  asubuhi
mpaka saa 4 na watakuwa wanapatikana kwa nambari 0657980000 ambapo amana Bank 
ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri kwa sasa wana matawi saba matano 
yakiwa Dar es salaam,Arusha,Mwanza na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoa 
mingi zaidi ila waliyoipa kipaumbele zaidi ni Zanzibar na Tanga


Akizungumza na waadishi wa habari meneja mfawidhi na huduma kwa wateja Juma Msabaha Amesema kuwa utaratibu
wanaotumia  kuweza kuwapata mawakala ni 
kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awe na tin namba ya biashara 
kuonyesha kuwa ni mlipa kodi  pia awe mefanya 
kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo 
ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza 
kujadiliwa na kama amekidhi vigezo atapewa uwakala ambapo amesema kuwa kwa sasa 
wana mawakala kwa mikoa kama tabora ,bukoba,na mtwara na bado wanaendelea 
kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.


Munir Rajab – mkuu wa idarara ya biashara amana benki amisema kuanzishwa kituo hicho kuna lengo la kuhitaji kuwa karibu na na wateja wao huku akitanabaisha  kuwa huduma za kibenki huwa zinafanana lakini 
kinachoweza kuwatofautisha ni ubora wa huduma kwa wateja na kwamba wao 
wamejipanga vizuri kuingia kwenye ushindani huo ambapo wameamua kuwa mwaka huu 
ni mwaka wa mawakala kwa sababu wanahitaji kuweza kuwafikia wateja wao mpaka 
mahali ambapo hakuna matawi na wataweza kutumia huduma za kibenki kupitia 
mawakala wao .
 Mkuu wa biashara wa Bank ya AMANA nchini Tanzania Munir rajab akieleza mambo mbalimbali kwa wanahabari kuhusu huduma hiyo mpya kutoka kwao

Bw. Juma Msabaha 
akijibu swali wa muandishi wa habari Alisema kuwa utaratibu wanaotumia  kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala 
lazima awe na leseni ya biashara pia awena tin namba ya biashara kuonyesha kuwa 
ni mlipa kodi  pia awe amefanya kazi zaidi 
ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni
0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza 
kujadiliwa na kana amekidhi vigezo atapewa uwakala . na kwa sasa wana mawakala 
kwa mikoa kama Tabora ,Bukoba,na Mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi 
kutoka kwa watu mbalimbali.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)