Kipindi cha The Mboni Show, chini ya Mtangazaji wake, Mboni Masimba ambacho kinachorushwa kupitia televisheni ya Taifa ya TBC, Jioni ya jana ya Juni 29.2016 wameweza kufuturisha wageni Watoto Yatima 268 kutoka katika baadhi ya vituo vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwafariji na kuwasaidia kama ilivyo kwa desturi ya waandaaji wa kipindi hicho huku Mama mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu.
Akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kufuturisha Watoto hao pamoja na wageni mbalimbali Mwanadada Mboni ameeleza kuwa, wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara hii ni kutokana na kurudisha fadhila kwa jamii kwa kidogo kinachopatikana hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kufanya jambo kama hilo kila inapohitajika kwa jamii.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amepongeza tukio hilo la Mwanadad Mboni Masimba kwani ni la kuigwa hivyo ni lazima jamii imuunge mkono kwa kujilea kwake.
"Nakupongeza Mboni na timu yako kwa kuwakumbuka watoto hawa. Tukio kama hili kuliandaa linahitaji gharama na kujitolea haswa. Tupo pamoja nawe na juhudi zako tunaziona nakupongeza sana." alibainisha Makamu wa Rais Mama Samia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, alimpongeza Mboni Masimba kwa shughuli hiyo kwani inasadia katika kukumbuka jamii hasa watoto hao ambao wengi wao wanalelewa katika vituo vya Yatima.
Katika tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee uliopo Posta jijni Dar es Salaam mbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, Pia viongozi wengine kadhaa walijumuika akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Mh Ali Hapi na viongozi wa dini Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum pamoja na Kaimu Mufti wa Tanzania aliyemwakilisha Mufti Mkuu pamoja na Mabalozi akiwemo Balozi wa INDIA.
Pia wadau wa kipindi hicho cha The Mboni Show, watu maarufu, Wasanii, Wanahabari na wadau wengine wakiwemo wadhamini waliofanikisha shughuli hiyo.


Baadhi ya wadau wakiwasilia kwenye tukio hilo kumpa kampani Mwanadada Mboni Masimba

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika tukio hilo




Baadhi ya watoto kutoka katika vituo vya kulea watoto Yatima ambao waliandaliwa futari hiyo maalum wakiwa katika tukio hilo

Mmoja wa wasomaji wa dini ya kiislamu akiendelea na dua


Wageni waalikwa wakiwa katika shughulo hiyo

Wadau


Dua zikiendelea



Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Mh. Ali Hapi akipata futari hiyo





Mwanadada Mboni Masimba akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo



Mkuu wa Mkoa wa Dar, Mh. Makonda



Mkuu wa Mkoa akiagana na wadau katika tukio hilo

Wadau waliojitokeza kumuunga mkono Mwanadada Mboni Masimba




No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa