Maonyesho ya bidhaa za Plastiki yaliyoanza jana Mei 27.2016 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam yanatarajia kufikia tamati hiyo kesho Jumapili ya Mei 29.
Maonyesho hayo ambayo Tanzania ni mwenyeji kwanza ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi yanakuwa ya kipekee huku watu mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.
Awali Meneja Mkuu wa Expo One, Ahmed Barakat ambao ni waandaaji wa maonyesho hayo, alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinashiriki katika maonesho hayo.
Afrika –PPB-EXPRO ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya na yatatoa mwanya wa kuyaelewa masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.
“Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha kuwa Tanzania ni ya kwanza katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.
Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara.
“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya biashara ya kimataifa pamoja na kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
Pichani juu ni baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL). Watu mbalimbali wamekuwa wkifika kwa wingi kwenye banda hilo kupata maelezo ya kina namna ya bidhaa bora za kampuni hiyo. Watu wote wanakaribishwa kufika kwenye banda hilo ambalo lipo mstari wa pili katika mlango wa kuingilia katika ukumbi huo.
Bwana Anwar Mohamed akitoa maelezo ya kina kwa baadhi ya wananchi waliokuwa wakitembelea maonyesho hayo katika banda la Talab.
Mwenyekiti wa kampuni ya Altalab Factories Group, kutoka Misri, Bw.Abdelhkim Altalab (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea katika banda hilo kwenye maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa kampuni ya Altalab Factories Group, kutoka Misri, Bw.Abdelhkim Altalab aliyeshika kiti, akimuonyesha mmoja wa wageni waliotembelea katika banda hilo kwenye maonyesho hayo.
Banda la bidhaa za Kiboko Alu-Zinc
Mwanadada Sarafina Wasley akitoa maelezo namna ya bidhaa zinazosambazwa na StoneBlock Bulding wakati wa maonyesho hayo.
Mwanadada Sarafina Wasley akitoa maelezo namna ya bidhaa zinazosambazwa na StoneBlock Bulding kwa wateja (hawapo pichani) wakati wa maonyesho hayo,
Meneja Masoko wa TCL (Technical Chemical Laboratory) , Bw Louay Abd El-Rahman (kushoto) akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesho hayo leo Mei 28.2016, katika ukumbi wa Mlimani City. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa