Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamewapongeza wasanii wa Tanzania kwa kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania nje ya mipaka kwa kufanya vizuri na kuibuka na ushindi ikiwemo tuzo katika filamu bora za Kiswahili zinazotoka Tanzania.
Akitoa pongezi hizo mapema leo 7 Machi.2016, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na wasanii mbalimbali wa filamu nchini waliowasindikiza washindi wa tuzo hizo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria,
Akiwemo mshindi wa tuzo ya filamu Bora ya Lugha ya Asili (Best Local Language -Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’, Msanii Single Mtambalike ‘Rich Rich’ pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba ambapo Waziri aliwapongeza kwa mshikamano wao huo waliouonyesha na hata kurudi kutoa pongezi.
Waziri Nape amebainisha kuwa, awali Rich Rich kabla ya kwenda Nigeria, alipata Baraka kutoka kwake hivyo hata kurejea kutoa shukrani ni jambo jema huku akieleza kuwa, Serikali itahakikisha inawalea wasanii katika umoja pamoja na kuweka mazingira mazuri ya ufanisi katika shughuli zao ikiwemo kuandaliwa Sera, kanuni na misingi ya sharia katika kuifanya tasnia ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi na yenye kuleta fursa za ajira kwa wasanii ndani na nje.
“Kwa nafasi yangu ya Uwaziri. Nitahakikisha nawapigania wasanii kufikia malengo tuliyoyakusudia. Hii ni pamoja na kuwa na Sera madhubuti na kuzuia mianya ya wafujaji wa kazi za Wasanii wa Tanzania. Serikali ya awamu ya tano kupitia kwa Rais wetu Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza na ili la stika za TRA
na munashuhudia wenyewe Mamlaka ya Mapato inavyopambana na watu wanaorudisha maendeleo ya wasanii nyuma kwa kufunga maduka yao huu ni mwanzo tutapambana mpaka mwisho katika hili” alieleza Mh.Nape na kupata pongezi kutoka kwa wasanii wenyewe ambao waliweza kushangilia kwa kauli hiyo ya matumaini huku wakipiga makofi.
Aidha, katika tukio hilo, Serikali imeweza kuwatunukia wasanii hao walioshinda tuzo hizo za AMVCA 2016 vyeti maalum vya shukrani hii ni pamoja na wasanii wote ambao filamu zao pia zilienda kushindanishwa huko pamoja na waandaaji waliowezesha filamu hizo kwa mchango wao mkubwa.
Katika tuzo hizo mbali na Rich Rich, kushinad tuzo hiyo, Msanii mwingine aliyeshinda ni pamoja na Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/Mo tv Online














No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa