Bei ya nishati ya mafuta imeendelea kushuka baada ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA kutangaza bei kikomo huku baadhi ya wananchi wakitaka bei za bidhaa nazo zishuke.
Akitangaza bei elekezi jijini Dar es Salaam mkurugenzi mkuu wa EWURA Bw.Felix Ngamlagosi amewataka wateja wa nishati ya mafuta kudai risiti pindi wanapopewa huduma hiyo na kwamba kuanzia sasa wananchi wanaweza kupata bei hizo kupitia simu zao za kiganjani.
Baadhi ya wananchi wameeleza kushangazwa na kitendo cha nishati hiyo kushuka mara kadhaa lakini bei za bidhaa kuendelea kupanda na kuitaka serikali kuunda tume ya bei huku wauzaji wa nishati hiyo wakielezea changamoto wanachokabiliana nazo katika kutoa risiti kwa wateja.
chanzo: ITV
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa