Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kuanza kutumia jokofu moja lenye uwezo wa kuchukua miili nane (8) katika chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) ya Hospitali hiyo baada ya kuridhishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kutembelea kwa mara ya pili kuikagua, tokea alipoipa masaa 72 ifungwe na ifanyiwe matengenezo.
Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa nane mchana na kisha kwenda moja kwa moja kwenye jengo hilo la Mochwari na kukuta mafundi wakiendelea na matengenezo kwa upande wa majokofu ambayo yalikuwa hayafanyi kazi na kusababisha matatizo hata Naibu Waziri kuagiza kufungwa siku tatu ili uongozi huo ufanyie matengenezo.
“Nilitoa masaa 72, muwe mumefanyia kazi tatizo hili. Na leo hii nimerudi tena kukagua kuona utekelezaji wa agizo langu kama mnalifanyia kazi. Hivyo kwa kuwa tayari ili jokofu moja limeanza kutengamaa nalifungulia lianze kazi mara moja na la pili lianze kazi pia litakapokamilika mutujulishe haraka sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Tumbi.
Ziara hiyo katika kukagua utekelezaji wa Mochwari hiyo ya Tumbi, ameifanya jana Machi 13.2016 akiambatana na maafisa wa Wizara yake hiyo ambapo pia alipata kutembelea Hospitali nyingine ya Jijini Dar es Salaam ya Sanitas ambayo imefungiwa kutoa huduma kwa upande wa chumba cha Upasuaji kutokana na kutokidhi vigezo.
Hata hivyo kwa upande wa Hospitali Dk. Kigwangalla alieleza bayana kuwa, alipata taarifa juu ya uongozi wa Hospitali hiyo kuendelea na huduma za upasuaji lakini hakukuta hali hiyo na kuendelea kusisitiza huduma hiyo isifunguliwe mpaka hapo watakapokamilisha vigezo vya Wizara juu ya Chumba chaa upasuaji kinavyotakiwa kiwe.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipatiwa maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi, Dk Dastan juu ya maendeleo ya majokofu hayo yanayofanyiwa ukarabati
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya majokofu ambalo limeharibika kwa muda mrefu kuona namna ya kuweza kulitengeneza ilikusaidiana na majokogu yaliyoppo sasa ambayo yanapokea miili 16.
Ukaguzi..
Fundi anayesimamia utengenezaji wa majokofu ya Hospitali ya Tumbi, Bw. Josiah Kulwa akimuonesha Naibu Waziri Dk. Kigwangalla jokofu hilo ambalo limeharibika muda mrefu. Hata hivyo Dk. Kigwangalla ametaka kuona uongozi wa Hospitaali hiyo unachukua hatua ya kufanyia matengenezo ililiweze kusaidia na majokufu mengine ilikuendana na hali halisi.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ukarabati wa majokofu hayo
Ukarabati..
Kifaa ambacho awali kilikuwa hakisomi kabisa na kubakia namba sifuri, baada ya ukarabati huo sasa kifaa hicho kimeanza kusoma kama kinavyoonekana pichani
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa fundi anayesimamia ukarabati huo
Ufuatiliaji ukiendelea..
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akiwa ameingiza mkono ndani ya jokofu hilo kama linafanya kazi ipasavyo. Hata hivyo jokofu hilo limeweza kutengamaa na kufanya kazi ipasavyo ambapo ameagiza lianze kufanya kazi.
Fundi anayesimamia utengenezaji wa majokofu ya Hospitali ya Tumbi, Bw. Josiah Kulwa akitoa maelezo namna ukarabati huo unavyoendelea..
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akiangalia namna utengenezaji huo unavyoendelea kwa upande wa nje wa majokofu hayo
Eneo la vifaa vya majokofu hayo ya Mochwari panavyoonekana wakati wa matengenezo hayo
Complesa ya zamani ambayo imeharibika ikiwa pembeni wakati wa matengenezo hayo
Matengenezo yakiendekea..
Fundi anayeshughulikia matengenezo hayo akimwelezea jambo, Dk Kigwangalla wakati alipowasili katika eneo hilo la Mochwari
Mtaalam wa upande wa Mochwari hiyo ya Tumbi akitafakari jambo wakati wa ujio huo wa Naibu Waziri Dk. kigwangalla
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akipokea taarifa na namna ya hatua zinazochukuliwa na Hospitali hiyo ya Tumbi, kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Dastan. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa